VIDEO: Real Madrid vs Liverpool ni haponi mtu Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

Kikosi cha Real Madrid kilitua Kiev,Ukraine  jana Alhamisi kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa kesho Jumamosi.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezungumzia mechi yao ya kesho dhidi ya Liverpool akisema matumaini makubwa ni kuibuka na ushindi utakaowafanya kunyakua taji hilo kwa mara ya tatu.
Kikosi cha Real Madrid kilitua Kiev,Ukraine  jana Alhamisi kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa kesho Jumamosi.
Kocha Zinedine Zidane ametua Ukraine akiwa na wazo moja la kutetea taji lake la ubingwa na kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo.
Liverpool wanatambua kwamba iwapo watafanikiwa kutwaa taji hilo msimu huu, watakuwa wameibuka mashujaa mbele ya wapinzani wao Real Madrid.