Ronaldo apiga nne Real yaua

Muktasari:

Real bado wanakibarua kizito cha kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Hispania msimu huu

Madrid, Hispania. Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya 50 katika maisha yake ndani ya Real Madrid baada ya kuichapa Girona bao 6-3 katika La Liga.

Ronaldo alifunga bao la kwanza akimalizia pasi ya Toni Kroos, lakini Cristhian Stuani aliwasawazishia Girona kufanya matokeo 1-1.

Real ilipata bao la pili lililofungwa na Ronaldo kabla ya kutegeneza bao la tatu lililofungwa na Lucas Vazquez na Mreno huyo kuongeza la nne.

Girona iliamka na kupata mabao yake mawili yaliyofungwa na Stuani na Juanpe, lakini mabingwa wa Ulaya, Real walithibisha ubora wao kuongeza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Gareth Bale na Ronaldo akihitimisha kalamu hiyo ya mabao.

Matokeo hayo yanaipeleka Rea hadi nafasi ya tatu wakiwa mbele ya Valencia, lakini wakiwa nyuma kwa pointi nne kwa mahasimu wao Atletico, ambao wamefungwa 2-1 na Villarreal.

Real bado wapo nyuma pointi 15, kwa vinara wa La Liga, Barcelona ambayo mapema jana ilishinda 2-0 nyumbani dhidi ya Athletic Bilbao.