Roma aomba Pooh!

Muktasari:

  • Msanii huyo ameomba apunguziwe adhabu hiyo au kutozwa faini ili aweze kuendelea na shughuli zake.

 Ziwa zimepita siku 20, tangu alipoanza kutumikia kifungo cha miezi sita cha kutojishughulisha na kazi za Sanaa, msanii wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Roma Mkatoliki’, msanii huyo ameomba apunguziwe adhabu hiyo au kutozwa faini ili aweze kuendelea na shughuli zake.

Roma ameyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha XXL kinachorushwa na kituo cha Radio Clouds ambapo alidai kuwa adhabu hiyo imekuwa na machungu kwange kutokana na kushindwa kufanya kazi na watu mbalimbali.

Msanii huyo amesema amamua kutumia kituo hicho kuomba msaha huo baada juhudi mbalimbali alizozitumika kutaka kukutana na Naibu Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza, aliyetengaza kumfungia Machi 1 mwaka huu kugonga mwamba.

Kauli hii ya Roma inapingana nay a Waziri Shonza ambaye juzi alikaririwa na gazeti la Mwananchi akisema kuwa msanii huyo alipoitwa kupewa nafasi ya kujitetea hakutokea na yeye hawezi kumlazimisha.

Akilijibu hilo, Roma amesema tangu siku alipofungiwa alijitahidi kufanya taratibu za kumuona Shonza kama ambavyo inasemwa kila wakati kuwa milango ya wizara iko wazi muda wote ikiwemo kufunga safari hadi kwa kiongozi huyo lakini hakufanikiwa.

Zaidi alisema hayo yametokea wakati akiwa tayari ana show za kufanya na alishachukua hela yake ikiwemo ya Kili Marathoni ambayo baadaye alitakiwa kurudisha.

Amesema “Show ya kili marathoni mimi na Stamini kupitia kundi letu la Rostamu tulikuwa tumelipwa vizuri lakini juhudi za kufanikisha ziligonga mwamba hata kwa kuomba barua kidogo ya utambulisho. Mambo kama haya yanatuharibia kuaminika tena kwa makampuni ambayo yanatupatia dili,”

 

 “Inaonekana Roma hajafanya kitu chochote tangu litokee jambo hilo lakini ambacho mimi sijafanya ni kuja kwenye media kusema leo nimeandika barua au vipi?, mimi sikupewa barua kwa wakati ule nilipewa ujumbe tena kwa namba ngeni ,” amesema Roma.

Kuhusu suala la wimbo wake wa kibamia ambao ndio ulikuwa chanzo cha kufungiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukaidi kuufanyia marekebisho, amesema tayari alikwisha rekebisha ili alikuwa anavizia upepo wa soko ndipo aweze kuiachia.