Rich Mavoco aishtaki WCB Basata

Hatimaye Uongozi wa WCB leo Jumanne umeweka wazi kuwa ni kweli Rich Mavoko ana matatizo na lebo hiyo na  tayari suala hilo limeshatua Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa WCB, Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kwa sasa asingeweza kuzungumzia kila kitu kwani ishu hiyo ipo BASATA ila wataongea rasmi baada ya maafikiano.

"Najua unakiu ya kuuliza maswali kuhusu Rich Mavoko, ila kwa sasa hatuwezi kuweka wazi  suala hili kwani limeshafika Basata. Tunatarajia kukaa kikao na Baraza hilo muda mfupi na baada ya hapo BASATA watatangaza rasmi maafikiano yatakayopatikana, hivyo haina haja ya kuficha kuwa hakuna tatizo na Rich," alisema Sallam

Wiki iliyopita Rich Mavoko alienda BASATA kulalamika kuwa mkataba wake na WCB unamnyonya na kulitaka Baraza hilo kuupitia upya.

Na leo Diaomond Platnumz na Mameneja wake wawili, Babu Tale na Sallam wametinga BASATA kuitikia wito wa baraza hilo kuhusu malalamiko ya msanii wa muziki Rich Mavoko aliyedai kuwa mkataba wake na WCB umekaa kinyonyaji.

Awali uongozi wa Wasafi waligoma kuweka wazi suala hilo.