Real Madrid yazoa Sh227 bilioni taji Ligi ya Mabingwa Ulaya

Baada ya Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/18, itaondoka na donge nono la takribani Sh227 bilioni.
Awali, Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) lilitangaza zawadi ya bingwa wa mashindano hayo msimu wa 2017/18 atajizolea Euro 100 milioni ambayo ni sawa na takriabani Shilingi 227 bilioni.
Msimu uliopita, Real Madrid ilinyakua taji hilo baada ya kuichapa Juventus kwenye mchezo wake wa fainali na kutetea taji hilo.
 Katika fainali hiyo ya mwaka 2017 Real Madrid walivuta mkwanja wa Euro 89.5 milioni.
Mashindano hayo ndiyo yanatajwa kuzipa timu kiasi kikubwa cha pesa ukilinganishwa na mashindano yoyoye yale duniani ya soka.