Real Madrid yamsaka Marcus Rashford

Muktasari:

  • Rais wa Real Madrid anaamini kumsajili Rashford au Kane itakuwa mbinu ya kumuongezea makali mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo.

Real Madrid imeweka wazi kwamba haitakuwa na huruma iwapo itashindwa kuidaka saini ya Harry Kane, kwani itapambana kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford.

Awali, Rais wa Real Madrid, Florentino Perez aliweka wazi kwamba yupo tayari kumsajili Kane kwa gharama yoyote na ikishindwana naye, Rashford ndiye atakuwa mbadala.

Hata hivyo, mpango wa Real Madrid kumsajili Kane unaonekana kuingia dosari baada ya klabu hiyo kuweka wazi kwamba haipo tayari kumuuza na iwapo kuna klabu, iende na Pauni 200 milioni kwenye meza ya mazungumzo.

Perez alisema kwamba klabu hiyo ikimnasa Rashford jambo hilo litapokewa kwa shangwe na mashabiki wa klabu hiyo pia mchezaji, Cristiano Ronaldo.