Real Madrid yamchefua Mo Salah, awapiga ‘stop’ kumsajili

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohammed Salah, ametoa ya moyoni ikiwa ni saa kadhaa kupita tangu beki wa Real Madrid, Sergio Ramos amsababishie majeraha yalimfanya atoke nje kipindi cha kwanza.
Mo Salah amesema baada ya kujeruhiwa na beki wa Real Madrid na kumharibia mchezo, hataweza kujiunga na klabu hiyo kutokana na kitendo ambacho siyo cha kiungwana alichofanyiwa jana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ukraine.
Salah ameeleza kusikitishwa zaidi na tukio la nahodha wa Real Madrid, Ramos kumuumiza mkono.
Mchezaji huyo amesema kitendo kama hicho ni mbinu chafu za kujitafutia matokeo badala ya kucheza mpira ambao unafuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.
Kuafuatia rafu iliyopelekea kuumia mkono wake, Salah amesema hataweza kujiunga na timu hiyo ambayo imeonesha nia ya dhati kutaka kumsajili hivyo ataendelea kubaki Liverpool na siyo kwenda Madrid.
Katika mchezo huo uliopigwa mjini Kiev, ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kubeba taji la tatu mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.