Real Madrid kufungia dirisha la usajili kwa Dea Gea

Hispania. Klabu ya Real Madrid imepanga kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea kutokana na kumkosa mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe.

Pia sababu nyingine inatajwa kuwa ni kutokana na kuimarika kwa kiwango cha Marco Asensio (21) jambo lililomshawishi kocha Zinedine Zidane kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji mwingine.

Taarifa zinaeleza kuwa, Real Madrid iliamua kuachana na Mbappe baada ya dau lake kuwa kubwa zaidi huku wakibadili mipango na kumhitaji De Gea.