Neymar kuifuata tuzo ya Ballon d’Or Real Madrid

Muktasari:

  • Ronaldo sasa ameshinda kwa mara nne Ballon d’Or akiwa Real Madrid na kuongeza ile moja aliyoipata wakati akiwa Manchester United

Rais wa Florentino Perez amechochea moto wa tetesi za uhamisho wa Neymar baada ya kusema nyota huyo angependa kushinda tuzo Ballon d’Or akiwa Real Madrid.

Perez alimsifu nyota wake Cristiano Ronaldo kwa kushinda tuzo ya tano ya Ballon d’Or, lakini alitumia nafasi hiyo kuwazungumzia wale wanaojaribu kufuata nyayo za nyota huyo.

“Ukiwa mchezaji wa Madrid inakuwa ni rahisi kwako kushinda Ballon d’Or,” alikiri hilo wakati alipoulizwa kuhusu Neymar.

“Real Madrid ni klabu inayokuwa kila kitu anachotaka mchezaji mkubwa, kila moja anajua hilo nilishataka kumsajili wakati fulani.”

Kwa sasa ameweka akili yake kwa mchezaji mwenye uwezo wa kuvunja rekodi ya ufungaji na kuchukua mataji kila mwaka.