RT kukusanya mamilioni

Muktasari:

RT juzi ilikutana na waandaaji wa mbio zote zinazofanyika nchini na kuwapa sheria mpya ya kuandaa mbio hizo huku kila mmoja akitakiwa kusajili upya mbio yake, kulipia ada na kila muandaaji kupeleka kalenda ya mbio yake kwenye kamati ya ufundi ya RT kabla ya Novemba 10.

Achana na zile Dola 15,000 ambazo Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limekuwa likipata kutoka kwenye Shirikisho la kimataifa (IAAF) kila mwaka, mabosi wa RT wataanza kukusanya kitita cha Sh122.5 milioni kila mwaka kupitia mapato ya mbio zinazofanyika nchini.

Iko hivi.

RT juzi ilikutana na waandaaji wa mbio zote zinazofanyika nchini na kuwapa sheria mpya ya kuandaa mbio hizo huku kila mmoja akitakiwa kusajili upya mbio yake, kulipia ada na kila muandaaji kupeleka kalenda ya mbio yake kwenye kamati ya ufundi ya RT kabla ya Novemba 10.

Rais wa RT, Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alisema sasa hizi mbio zote zinazofanyika nchini zitakuwa katika madaraja na tayari wamezigawa kwenye madaraja manne tofauti ambapo sasa daraja la kwanza litakuwa na mbio tisa, daraja la pili mbio tatu, daraja la tatu mbio tano na daraja la nne mbio 10.