QPR waogelea maji machafu

MECHI ya kirafiki kati ya QPR na Union Berlin kule Ujerumani ilikatizwa katika dakika ya 13 kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wikiendi iliyopita, achana na hilo!

Stori ni kwamba baada ya mechi kukatishwa wachezaji waligundua kuwa mashabiki walikuwa na kiu kubwa ya burudani na wakaamua kuanza kuogelea katika maji machafu yaliyojaa uwanjani ikiwa ni ishara ya kuwafurahisha mashabiki.

 Wachezaji wa timu hizo walianza kuogelea kila upande ambapo mashabiki walilipuka kwa furaha na kuanza kuwashangilia. Mechi hiyo iliamuriwa kurudiwa wiki hii.