Prisons yajipigia hesabu kuchukua pointi zote Kanda ya Ziwa

Muktasari:

Asukile alisema msimu uliopita walipata wakati mgumu baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi tano walizocheza kanda ya ziwa  hivyo msimu huu wanataka kulipa kisasi.

Dar es Salaam. Baada ya kuitandika Mwadui mabao 3-1 jana Jumamosi, mchezaji wa Prisons, Benjamini Asukile  amesema wamedhamiria msimu huu kuhakikisha wanaondoka na pointi zote katika mechi watakazocheza Kanda ya Ziwa.

Asukile alisema msimu uliopita walipata wakati mgumu baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi tano walizocheza kanda ya ziwa  hivyo msimu huu wanataka kulipa kisasi.

Msimu uliopita,Prisons ilichapwa na Mwadui bao 1-0, ikafungwa na Kagera Sugar mabao 2-0, ikanyukwa na Mbao bao 1-0, kisha ikachapwa na Stand United bao 1-0 halafu ikatoka sare ya 1-1 na Toto Africans.

Alisema, "Msimu uliopita tulipata wakati mgumu sana  katika mecho zote tulizocheza kanda ya ziwa, tulipoteza karibu pointi zote.”