Pointi moja tu yawapa Ndanda Sh 2 milioni

Muktasari:

Ndanda imeifunga Simba bao 1 tu katika michezo tisa waliyokutanaNdanda imeifunga Simba bao 1 tu katika michezo tisa waliyokutana

Mtwara. Kitendo cha Ndanda kuandika rekodi ya kuvuna pointi ya kwanza mbele ya Simba, imewafanya wachezaji wa timu hiyo kuvuna Sh 2 milioni.

Ndanda wakiwa kwenye Uwanja wao wa Nangwanda Sijaona, mjini hapa ilipewa fedha hizo na Mkuu wa Mkoa huo, Gelasius Byakanwa kama asante ya kuvuna kwa mara ya kwanza pointi mbele ya Mnyama.

Kwa misimu minne mfululizo ikicheza mechi nane, Ndanda ilikuwa haijawahi kuambulia japo sare mbele ya Simba na badala yake ilikuwa ikifumuliwa, huku yenyewe ikiambulia bao 1 kati ya 19 iliyoruhusu kufungwa na Wekundu hao.

Lakini jioni ya leo, Ndanda chini ya Kocha Hamis Malale 'Hamsini' ililazimisha suluhu na kupata pointi moja iliyoifanya ifikishe alama 4 kutokana mechi nne ilizocheza mpaka sasa katika ligi ya msimu huu wa 2018-2019.

Kufuatia suluhu hiyo, RC Byakanwa aliamua kuwazwadiwa wachezaji wa timu hiyo akiwapongeza kwa walichokifanya Nangandwa.

 

Rekodi zilivyo

2014-2015

Ndanda 0-2 Simba (Sserunkuma, Elias Maguri)

Simba 3-0 Ndanda (Mkude, Singano, Ndemla)

2015-2016

Ndanda 0-1 Simba (Ajibu)

Simba 3-0 Ndanda (Kazimoto,Kiiza (2)

2016-2017

Simba 3-1 Ndanda (Mavugo, Blagnon, Kichuya; Mponda)

Ndanda 0-2 Simba (Mzamiru, Mo Ibrahim)

2017-2018

Ndanda 0-2 Simba (John Bocco (2)

Simba 1-0 Ndanda (Okwi)