Pogba hata Griezmann akicheze Man City kwangu poa tu

Muktasari:

  • Lakini ameamua kusaini mkataba mwingine  wa muda mrefu na Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufungiwa na Fifa kusajili.

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesisitiza atakuwa mwenye furaha endapo Antoine Griezmann atajiunga na Manchester City.

Griezmann amekuwa akihusishwa na kuunga na Pogba ndani ya Manchester United msimu huu.

Lakini ameamua kusaini mkataba mwingine  wa muda mrefu na Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufungiwa na Fifa kusajili.

Pogba alisema atakuwa mwenye furaha na Griezmann akichagua kucheza sehemu yoyote anayopenda.

Pogba aliimbia Telefoot: “Griezmann? Namtakia mafanikio mema. Kama atacheza Atletico, au Man City, nitakuwa tayari kupokea hilo. Yeye ni mchezaji bora duniani kwa sasa.