Pogba anatakata hadi aibu

Muktasari:

  • Kiungo huyo Mfaransa amerejea kutoka katika majeruhi na kuonyesha kiwango cha juu

London, England. Paul Pogba amethibitisha thamani yake ya kununuliwa Pauni 89 milioni kutoka kwa ‘Kibibi Kizee’ cha Turin Juventus.

Mwishoni mwa wiki kiungo huyo alicheza soka ya maana katika mchezo ambao Man United ilitoka nyuma na kushinda mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United.

Pogba alifunga bao la tatu katika mchezo  alicheza kwa kiwango bora nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alicheza mchezo wa kwanza akitokea katika maumivu ya misuli yaliyomuweka nje ya uwanja muda mrefu.

Pogba alikuwa chachu ya ushindi katika mchezo huo ambao United ilianza kwa kuchapwa bao 1-0 kabla ya kuondoka na karamu ya mabao.

Newcastle United ilionekana kutawala dakika 45 za mwanzo, lakini Man United ilizinduka huku Pogba akicheza kwa kiwango bora.

Pogba alifanya kazi ya ziada kuunganisha safu ya kiungo akicheza pacha na Nemanja Matic.