Pogba amhurumia Neymar kelele za mashabiki asipofunga mabao

Muktasari:

  • Pogba alisema sasa mzigo huo ameupokea Neymar ambaye anashikilia rekodi ya mchezaji ghari kusajiliwa na PSG kwa thamani ya Pauni 198 milioni msimu wa 2017/18.


England. Mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba (24) amesema msimu uliopita alipata kashikashi ya mashabiki kutokana na kila mtu akimhusisha na thamani yake ya usajili na kiwango cha uwanjani.

Pogba alisema sasa mzigo huo ameupokea Neymar ambaye anashikilia rekodi ya mchezaji ghari kusajiliwa na PSG kwa thamani ya Pauni 198 milioni msimu wa 2017/18.

Neymar alikuwa Paris Ufaransa ambako mashabiki wa PSG walijumuika kushehekea uhamisho wake, huku akitumia nafasi hiyo kupiga mpira kwenye kiti maalumu alichoandaliwa,  ambapo fedha zitakazopatikana kwenye sherehe hiyo zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko Siera Lione.