Duh! Pluijm, Ngoma, Azam mbona raha!

Muktasari:

Katika kipindi cha ligi kuu msimu uliopita, Ngoma ameichezea Yanga wakaachana mwanzoni mwa mwezi Mei.

Dar es Salaam. Kama ulikuwa hujui 'inshu' ya Mzimbabwe Donaldo Ngoma na Azam FC basi iko hivi.
Ngoma ambaye amemalizana na Azam akitokea Yanga inadaiwa kuwa uwepo wake ndani ya klabu hiyo umefanikishwa na Kocha Hans Van Pluijm.
Pluijm anayedaiwa kuwa ndiye atakuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kwa msimu ujao, anamjua vizuri Ngoma.
Kocha huyo Mholanzi alimfundisha Ngoma ndani ya kikosi cha Yanga kabla ya kwenda kuinoa Singida,  pia  ndiye aliyefanikisha usajili wa Mzimbabwe huyo kutua kwa Wanajangwani hao akitokea FC Platinum ya nchini humo.
Inadaiwa Pluijm ameshawapa Azam mapendekezo yote ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika msimu mpya wa ligi kuu na usajili ni miongoni mwa vitu hivyo.
Katika kipindi cha ligi kuu msimu uliopita, Ngoma ameichezea Yanga na alimalizana nayo mwanzoni mwa mwezi Mei.