Pawasa aitonya Simba, mashabiki wanataka mabao tu

BEKI wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amewataka mastaa  wa timu hiyo, kutambua  mapema kwamba mwamko walionao mashabiki wao, unahitaji faraja ya ushindi katika mechi za ligi.

Anasema kama mashabiki wanaumizwa na matokeo ya mechi za kirafiki, mastaa wa kikosi hicho wajue wazi ya ligi yatakuwa zaidi, hivyo amewasisitiza kujiwekea malengo ya kila mechi.

"Ujue Simba na Yanga hazina mechi ya kirafiki, mashabiki wanahitaji kuona timu zao zinashinda kila zinapocheza, hilo liwe alama kwa wachezaji kufunzwa na mwamko wa mashabiki wao kwamba unahitaji faraja.

 "Ndio maana unasikia watu wanazimia uwanjani, inatokana na mashabiki wanakuwa wameandaa kupokea faraja, lakini mwisho wa picha wanakuwa wanaambulia maumivu, hivyo waanze kuandaa akili zao kujitoa kwa ajili ya timu ili kutimiza kile ambacho kimewafanya wawe Msimbazi,"anasema.