Paris Saint-Germain yaingia vitani na Barcelona kuisaka saini ya Dembele

Muktasari:

  • Mataji hao wa Ufaransa wameshindwa kuipata saini ya Alexis Sanchez na Kylian Mbappe, lakini rais wake Nasser Al-Khelaifi anamini itakuwa jambo jema kuipata saini ya Dembele (20).

Paris, Ufaransa. Paris Saint Germain, imeingia anga za Barcelona kwa kutangaza nia yao ya kumtaka Ousmane Dembele na kutishia uwezeko wa nyota huyo kutua Camp Nou.

Mataji hao wa Ufaransa wameshindwa kuipata saini ya Alexis Sanchez na Kylian Mbappe, lakini rais wake Nasser Al-Khelaifi anamini itakuwa jambo jema kuipata saini ya Dembele (20).

Kwa mujibu wa L'Equipe, iliyotoa taarifa ya  Dembele katika ukurasa wake wa mbele Jumatatu, imesema PSG tayari imeshafanya mawasiliano na wakala la mchezaji huyo.

Hata hivyo uhamisho huo bado ni mgumu baada ya mkurungezi wa ufundi wa Borussia Dortmund, Michael Zorch kusema mchezaji huyo ataendelea kuvaa jezi ya njano msimu ujao.