Pamba yasuka timu upya

Monday November 13 2017

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Kocha Msaidizi wa Pamba SC, Salmin Kamau amesema kuwa ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo iliyobaki ya ligi daraja la kwanza watasajili wachezaji wawili mshambuliaji  na kipa.

 Pamba iliyoanza vibaya ligi hiyo, ilifufuka katika mechi za mwisho na kufanikiwa kukaa nafasi ya nne kwa pointi 12 baada ya mechi tisa kwenye Kundi C.

 Kocha Kamau alisema ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri, wataongeza wachezaji wawili katika safu ya ushambuliaji na kipa na wenye uzoeufu na ligi.

 Alisema wamebaini hali ya ushindani, hivyo kwa kipindi cha mapumziko watakitumia vyema kuhakikisha wanaziba mapungufu yaliyoonekana.

 “Tumebaini kwamba ligi inahitaji ushindani, kwahiyo sisi Pamba tutaongeza wachezaji wawili, mshambuliaji mmoja na Kipa mmoja wenye uzoefu wa ligi,” alisema Kamau.