Pacha ya Makambo, Ajibu kuimaliza Stand

Muktasari:

  • Inaingia uwanjani ikiwa na mshambuliaji wao tegemezi, Mkongo Harieter Makambo ambaye alishindwa kumaliza mchezo uliopita kutokana na maumivu na atakuwa pacha wa Ibrahim Ajib.

Dar es Salaam. Ligi Kuu Bara inaendelea leo Jumapili wakati Yanga ya jijini Dar es Salaam, itakapoikaribisha Stand United kwenye Uwanja wa Taifa na Mbeya City itacheza na Alliance FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga ambao ni timu pekee iliyocheza mechi moja tu walipoifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 tofauti na nyingine, kutokana na kubanwa na ratiba ya mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.

Inaingia uwanjani ikiwa na mshambuliaji wao tegemezi, Mkongo Harieter Makambo ambaye alishindwa kumaliza mchezo uliopita kutokana na maumivu na atakuwa pacha wa Ibrahim Ajib.

Wawili hao ndiyo watakaoing'arisha safu ya ushambuliaji katika mchezo huo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amewasisitizia wachezaji wake kuwa mchezo wa kasi na pasi za haraka itakuwa njia rahisi ya wao kuibuka na ushindi mnono.

Katika mchezo wa Uwanja wa Sokoine, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Nsanzurwimo Ramadhani amesema, watahakikisha wanaibuka na ushindi baada ya kupoteza mechi zote tatu walizocheza ugenini.

"Hii ni nafasi pekee kwetu, tuko nyumbani na hivyo tunatakiwa kwa namna yoyote ile tunatakiwa kuwafunga Alliance.