Ditram Nchimbi aanza kazi Azam

Muktasari:

  • Klabu nyingi zilikuwa zikinihitaji ikiwemo Yanga pamoja na KMC  lakini naweza kusema Azam ndio tulielewana, wengine walikuwa wanapiga simu na kunambia niendelee kusubili lakini kwa upande wa hawa jamaa waliniita moja kwa moja njoo na nikakamilisha kila kitu.

Dar es Salaam: Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Ditram Nchimbi amesema sababu kubwa ya yeye kukubali kutua katika kikosi hicho ni umakini waliouonyesha katika kumsaka tofauti na klabu nyingine ambavyo vilikuwa vikisuasua.

“Klabu nyingi zilikuwa zikinihitaji ikiwemo Yanga pamoja na KMC  lakini naweza kusema Azam ndio tulielewana, wengine walikuwa wanapiga simu na kunambia niendelee kusubili lakini kwa upande wa hawa jamaa waliniita moja kwa moja njoo na nikakamilisha kila kitu.

KMC wao  pia walionyesha utayari lakini walijivuta” amesema Nchimbi.

Akizungumzia nafasi yake ndani ya kikosi hicho ambacho kina washambuliaji wengi na ushindani umeongezeka zaidi baada ya Donald Ngoma kujiunga na timu hiyo.

“Binadamu huwa tupo tofauti hata kama mnafanana, kikubwa mpaka wananisajili kuna

kitu walikiona kwangu kwa hiyo naahidi sitowaangusha na tukiwa na kikosi kipana kama hivi

ndio itakuwa chachu kubwa ya mafanikio kwao na kwangu lakini pia napenda niende sehemu

yenye changamoto ili nipambane,” aliongeza.

Nchimbi aliongeza kwamba atakuwa hana ugeni katika kikosi hicho kutokana na kufahamiana

vizuri na Joseph Mahundi na Idd Kipagwile ambao waliwahi kucheza katika timu ya Majimaji

Songea, huku wote wakitokea Ruvuma.