PSG yakata dau dogo la Juventus walilitoa ili kumnasa Matuidi

Muktasari:

  • Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi kwa sasa anasubili kumsikia Matuidi mwenyewe kama anataka kuachana na klabu hiyo ya Ligue 1.

Gazeti la L'Equipe limesema kuwa Paris Saint-Germain imekataa dau la pauni13milioni ilizotolewa na Juventus kwa ajili ya kumsajili Blaise Matuidi.

Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi kwa sasa anasubili kumsikia Matuidi mwenyewe kama anataka kuachana na klabu hiyo ya Ligue 1.

Ni Al-Khelafi pekee anayetaji kusikia kauli ya Matuidi kabla ya kuamua kuuza kiungo huyo mwenye miaka 30.