PSG wagundua Luis Enrique anaenda Chelsea

PARIS, UFARANSA
MABOSI wa Paris Saint-Germain wameshakubaliana na hali halisi kwamba kocha wanayemsaka Luis Enrique atatimkia Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Antero Henrique alikuwa na mpango wa kumvuta kocha huyo wa zamani wa Barcelona kwenye kikosi chake na kumpiga chini Unai Emery.
Lakini taarifa zinadai bosi huyo ameshaambiwa kila kitu kuwa Enrique amekubali dili la kwenda kuinoa Chelsea na kinachosubiriwa ni msimu tu umalizike akarithi mikoba ya Antonio Conte.
Kutokana na hilo, PSG sasa itakuwa na nafasi ya kumchukua Conte kama itahitaji huduma yake, huku taarifa za karibuni zikidai wababe hao wa Ufaransa wamekuwa wakipiga hesabu za kuinasa huduma ya Mtaliano huyo ili akawafanye kuwa bora zaidi na kushindana kwenye michuano mikubwa kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

...