PGS waitaka Manchester United kubadilishana Antony Martial vs Marco Verratti

Muktasari:

  • Jose Mourinho amejipanga kumsajili Verratti (24) ikiwa ni mshambuliaji wa tatu anayetajwa kutengewa fedha nyingi katika usajli wa msimu huu wa kiangazi.

 Klabu ya PSG imeieleza Manchester United kwamba nao wanamhitaji Anthony Martial ikiwa ni sehemu ya mkataba wao iwapo wanataka kumchukua Marco Verratti.

Jose Mourinho amejipanga kumsajili Verratti (24) ikiwa ni mshambuliaji wa tatu anayetajwa kutengewa fedha nyingi katika usajli wa msimu huu wa kiangazi.

PSG imetenga Pauni 60 milioni kwa ajili ya kuidaka saini ya kiungo Martial. Pia Barcelona imekuwa ikitajwa kumnyatia mchezaji huyo ambaye PGS wanamhangaikia kwa kila namna ili wamnase.