Oxlade-Chamberlain hatihati Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kiungo huyo aliumia dakika ya 20 katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Liverpool ilishinda mabao 5-2 dhidi ya AS Roma ya Itali.

LONDON, ENGLAND

ALEX Oxlade-Chamberlain ameweka rehani matumaini ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata maumivu

makali ya goti.

Kiungo huyo aliumia dakika ya 20 katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Liverpool ilishinda mabao 5-2 dhidi ya AS Roma ya Itali.

Kocha Jurgen Klopp amethibitisha mchezaji huyo ameumia vibaya na anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Fainali za Kombe la Dunia zimepangwa kuanza Juni 14 nchini Russia na Oxlade-Chamberlain anaweza kushindwa kuiwakilisha England.

Oxlade-Chamberlain ameanguka mara mbili ndani ya dakika 20 kabla ya nafasi yake kujazwa na Georginio Wijnaldum baada ya kuumia goti la mguu wa kulia alipogongana na Aleksandr Kolarov.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, alizungukwa na baadhi ya wachezaji wenzake huku akiwa ameshika sehemu ya goti.

Klopp ameingia hofu kama mchezaji huyo anaweza kurejea katika kiwango chake wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City.