Omog haachi mchezaji msimu huu

Muktasari:

Omog ambaye jana Jumanne, alikutana na kamati ya usajili ya Simba kujadili ripoti yake ya wachezaji ambao anataka wasajiliwe katika usajili wa dirisha dogo, ndipo akaisisitizia kamati hiyo mpango wake wa kutoacha mchezaji.

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amewapiga biti wachezaji wake na kuwaambia hataki hata mmoja aondoke katika kikosi hicho kwani wote bado wapo katika mipango yake ya msimu huu.
Omog ambaye jana Jumanne, alikutana na kamati ya usajili ya Simba kujadili ripoti yake ya wachezaji ambao anataka wasajiliwe katika usajili wa dirisha dogo, ndipo akaisisitizia kamati hiyo mpango wake wa kutoacha mchezaji.
Meneja wa Simba, Richard Robart alisema, kocha hajapendekeza jina la mchezaji yeyote kuachwa na kama kuna ambaye atataka kuondoka, basi ni kwa mahitaji yake mwenyewe.
“Hatujaanza kusajili na kama tutasajili basi si zaidi ya wachezaji wawili kutoka na upana wa kikosi chetu kilivyo, ndio maana hata kocha amesisitiza kubaki na wachezaji wote kwani licha ya wengine kutokucheza ni muhimu kwake,” alisema Robart.