Olympiakos yamtaka Emenike yamtosa Mbokani katika usajili wake

Muktasari:

  • Taarifa ya vyombo vya habari vya Ugiriki na Uturuki vimedai kuwa Olympiakos na Emenike wamefikia makubaliano binafsi, na klabu hiyo ipo tayari kutoa euro 2 milioni wiki hii kumsajili.

London, England. Mabingwa wa Ugiriki, Olympiakos wapo katika mazungumzo na mshambuliaji wa Nigeria, Emmanuel Emenike anayechezea  Fenerbahce.

Taarifa ya vyombo vya habari vya Ugiriki na Uturuki vimedai kuwa Olympiakos na Emenike wamefikia makubaliano binafsi, na klabu hiyo ipo tayari kutoa euro 2 milioni wiki hii kumsajili.

Miamba hiyo ya Ugiriki inamtaka mshambuliaji huyo baada ya kuuza Mnigeria mwingine, Brown Ideye kwa klabu ya China ya Tianjin Teda mwezi Februari mwaka huu.

Pia, alikuwa wakimtaka mshambuliaji wa DR Congo, Dieumerci Mbokani, lakini uhamisho huo ulikwama baada ya kushindwa katika vipimo vya afya.