Nyota watatu wafukuzia mchezaji bora England

England. Nyota watatu wa England wamekoleza mbio za kuwania nafasi ya mfungaji bora msimu huu kwenye Ligi Kuu England, huku kila mmoja akiamini ataibuka wa kwanza.

Kevin De Bruyne, Mo Salah na Harry Kane wamekuwa kwenye mbio hizo baada ya kuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu.

De Bruyne ukimlinganisha na Salah pia wamekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu jambo ambalo linaonekana wanaweza kufuta ndoto ya Kane ambaye naye ana matumaini makubwa ya kuwashinda wenzake.

Mbio hizo za kufuzia mchezaji bora zimewakatisha tamaa nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez na Paul Pogba ambao walitarajiwa kufanya makubwa msimu huu lakini mambo yanaonekana hayajawaendea vyema.

Hali sio mbaya tu kwa wachezaji wa Man United waliokata tamaa, lakini inaonyesha kwamba hata kocha Jose Mourinho amekosa matumaini ya kuwa kocha bora wa msimu huu.