Nyota wanne hawajatambulishwa Simba Day

WACHEZAJI Juuko Murshid na Haruna Niyonzima, Salim Mbonde na Said Mohammed 'Nduda', hawakuwepo katika orodha ya wachezaji waliokuwa wanatambulishwa katika utambulisho wa wachezaji wa Simba.

Katika utambulisho huo mashabiki wengi walitarajia kuona na kusikia majina hayo lakini hali ilikuwa tofauti.

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manar, alimaliza kuita orodha ya wachezaji hao kwa kuhitimisha kwa jina la mshambuliaji John Bocco, hali iliyofanya mashabiki kuanza kujiuliza kuhusu wachezaji wao Niyonzima na Juuko.

Awali iliripotiwa kwamba Haruna Niyonzima yupo nyumbani kwao nchini Rwanda licha ya kukatiwa Visa ya kwenda nchini Uturuki huku Juuko Murshid ambaye alikuwa akifanya majaribio nchini Afrika Kusini nar akikosekana uwanjani hapa.

Wakati huo huo Salim mbonde anasumbuliwa na Majeruhi huku Said Mohammed 'Nduda' ikiwa bado haijajulikana nini shida kwani mchezaji huyo hakuwepo hata katika kambi ya nchini Uturuki.

Hali hiyo imezidi kuzua hoja kwa mashabiki kwani wamejikuta wakiulizana maswali yasiyo na majibu kama wachezaji hao bado ni wa kwao au vipi.