Nyota wa Chelsea Hazard ni mwendo wa bata tu!

Muktasari:

  • Hazard ambaye aliiongoza timu yake ya taifa ya Ubelgiji, alionyesha kiwango cha kuvutia na kufanikiwa kuondoka na medali ya shaba kwenye mashindano hayo baada ya kumaliza mshindi wa tatu.

Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ametua nchini Hispania kwa ajili ya mapumziko mafupi ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Russia.
Hazard ambaye aliiongoza timu yake ya taifa ya Ubelgiji, alionyesha kiwango cha kuvutia na kufanikiwa kuondoka na medali ya shaba kwenye mashindano hayo baada ya kumaliza mshindi wa tatu.
Nyota huyo amepokewa kishujaa nchini mwake kutokana na kuonyesha kiwango cah kuvutia kwenye mashindano hayo ya Kombe la Dunia ambayo Ufaransa imeondoka na taji la ubingwa wa dunia.
Hazard mwenye miaka 27, ametua Hispania kwenye mapumziko huku nyota huyo akihusishwa na kuhamia klabu ya Real Madrid.
Mbelgiji huyo alionekana akiwa amepiga picha na mashabiki wake ambao ni raia wa Norway kwenye moja ya fukwe nchini humo.