Nyoni kama Mjeshi aisee

Muktasari:

Nyoni ambaye yupo pia kwenye kikosi cha Taifa Stars, amekuwa akicheza nafasi za beki wa kulia, kushoto, katikati pamoja na kiungo jambo ambalo linamfanya kuwa mchezaji wa kipekee zaidi nchini.

KIRAKA wa Simba, Erasto Nyoni ni mbishi usiambiwe na mtu na kwa kuthibitisha hilo jamaa amekuwa akitumika katika maeneo karibu yote uwanjani, lakini mwenyewe anasema ni poa tu kwani yuko imara kama chuma.

Nyoni ambaye yupo pia kwenye kikosi cha Taifa Stars, amekuwa akicheza nafasi za beki wa kulia, kushoto, katikati pamoja na kiungo jambo ambalo linamfanya kuwa mchezaji wa kipekee zaidi nchini.

Mwanaspoti lilimtafuta na kutaka kufahamu ugumu ambao anakutana nao pindi anapocheza katika mifumo tofauti, sasa sikia alichokisema.

“Mimi ni kama mwanajeshi na siku zote mwanajeshi aliye kamili huwa fiti dakika zote na anachokifanya yeye ni kufuata amri anayopewa, ndivyo nilivyo na mimi. Katika mfumo wowote nacheza tu,” alisema Nyoni ambaye kwenye mechi ya Taifa Stars na Algeria aliingia kipindi cha pili kucheza nafasi ya kiungo.