Nyanza wanusa hujuma michuano Ligi ya Mabingwa Mikoa

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa Timu hiyo Daniel Ndaikya alisema kuwa michezo hiyo ilipangwa kuanza muda mmoja ili kuepuka tatizo hilo kutokana na timu tatu kuwa zimewiana alama zote zikiwa na pointi 11 huku zikitofautiana mabao.

Arusha. Uongozi wa timu ya Nyanza FC iliyokuwa inashiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) kituo cha Tabora iliyomalizika mwishoni mwa wiki, umesema kuna dalili za upangaji wa matokeo.

Katibu Mkuu wa Timu hiyo Daniel Ndaikya alisema kuwa michezo hiyo ilipangwa kuanza muda mmoja ili kuepuka tatizo hilo kutokana na timu tatu kuwa zimewiana alama zote zikiwa na pointi 11 huku zikitofautiana mabao.

Ndaikya alisema kuwa pamoja na kupangwa muda mmoja kuanza kwa Michezo hiyo, lakini mchezo kati ya Area C na Green FC ulichelewa dakika kumi wakisubiri mchezo wao dhidi yao na Bodaboda uanze.