Nonga, Luhende sio ishu kabisa

Muktasari:

Akizungumza na Mwanaspoti, Bizimungu alisema amewaaminisha vijana wake kuwa, wanaweza na hiyo ndio siri kubwa ya Mwadui kuonyesha uwezo katika michezo kadhaa waliyocheza hadi sasa.

KUONDOKA kikosi kwa baadhi ya nyota waka akiwamo Paul Nonga, David Luhende na Abdallah Mfuko kumeelezwa wala sio ishu sana Mwadui kwa vile waliziba nafasi yao wanafanya vema.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ally Bizimungu alisema atalitupia diorisha dogo lijalo Novemba mwaka huu kuongeza mashine nyingine mpya ili chama lao likae vyema katika Ligi Kuu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bizimungu alisema amewaaminisha vijana wake kuwa, wanaweza na hiyo ndio siri kubwa ya Mwadui kuonyesha uwezo katika michezo kadhaa waliyocheza hadi sasa.

Alisema tatizo kwa sasa ni kuunganisha timu kucheza pamoja ndio maana wamejikuta wakiambulia alama moja tu katika mechi tatu walizocheza mpaka sasa katika ligi hiyo. Bizimungu alisema ni kweli timu yao imeondokewa na baadhi ya nyota, lakini tayari wamepata wa kuchukua nafasi zao.

“Kwa mfano nafasi ya Paul Nonga tumemnasa kijana Innocent Edwin ambaye alionekana kuwa mwiba katika mchezo wao dhidi ya Azam (ndiye aliyefunga bao la kusawazisha),” alisema.