Noma! Adili kuwania namba England

Adi Yussuf

Muktasari:

  • Moors imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa Cheltenham Town, Daniel Wright kwa uhamisho wa dau la Euro 50,000 Mshambuliaji huyo, anatarajiwa kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo msimu uliopita ilikuwa ikiongozwa na Adi.

MSHAMBULIAJI wa Kitanzania, Adi Yussuf mwenye asili ya visiwani Zanzibar ameletewa mshindani kwenye klabu yake ya Solihull Moors F.C inayoshiriki Daraja la tano England.

Moors imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa Cheltenham Town, Daniel Wright kwa uhamisho wa dau la Euro 50,000 Mshambuliaji huyo, anatarajiwa kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo msimu uliopita ilikuwa ikiongozwa na Adi.