Njombe Mji wafuta kumbukumbu mechi ya Yanga

Monday September 11 2017

 

By Olipa Assa

Kocha msaidizi wa Njombe Mji, Mlage Kabange  amesema kwa sasa wamezipa kisogo habari za Yanga, kinachowaumiza akili ni mchezo wao dhidi ya Mbeya City, iliyotoka kufungwa na Ndanda FC.

"Ni kweli Yanga, wamevuna pointi tatu kwetu, lakini nadhani watakuwa wamelala na viatu kwa kazi ambayo imeonyeshwa na vijana wetu ambao gharama za usajili na matunzo tofauti na wao," anasema.

Mlage alisema wanaelekeza nguvu kuhakikisha mchezo wao na City, angalau wanaambulia chochote kitakachowapa taswira ya mbele kitakachowapa moyo mashabiki wa timu hiyo.

"Njombe Mji ndiyo kwanza imeanza kucheza Ligi Kuu, kupoteza mechi mbili nyumbani imewaumiza mashabiki, lazima tupambane kuhakikisha tunafuta machungu yao, inawezekana kuwafunga City, kwao mbona Ndanda wameweza,"alisema.