Ngumi za Joshua zavunja dirisha Uholanzi

Muktasari:

Joshua bingwa wa uzito wa juu duniani anayeshikilia mataji mawili ya IBF na WBA.

AMSTERDAM, UHOLANZI. Bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua, amezindua duka kwa staili ya aina yake mjini Amsterdam, Uholanzi.

Joshua bingwa wa uzito wa juu duniani anayeshikilia mataji mawili ya IBF na WBA, alizindua duka hilo kwa kupiga ngumi mbili kali zilizovunja dirisha la vioo.

Lakini, uzinduzi huo ulikuwa ni sehemu ya kunogesha Kampuni ya Marekani Under Armour inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo ambapo Joshua ni miongoni mwa wadhamini wake.

Bingwa huyo wa dunia, yuko nje ya ulingo tangu alipomchapa Carlos Takam, katika pambano lililochezwa Oktoba, mwaka huu.

Tukio hilo la Joshua mwenye miaka 28, lilihudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki. Joshua ameshinda mapambano 20 yote kwa KO.