Ngoma kimeeleweka Azam

Muktasari:

Matajiri hao wa Azam baada ya 'dili' lao kukamilika, wameamua kabla ya kuanza kucheza, watampeleka nchini Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo zaidi.

Dar es Salaam: Azam FC imefanya kweli baada ya kumalizana na Mzimbabwe Donaldo Ngoma.
Matajiri hao wa Azam baada ya 'dili' lao kukamilika, wameamua kabla ya kuanza kucheza, mchezaji huyo atapelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo zaidi.
Ngoma ataanza kuichezea timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2012-2013 katika kipindi cha msimu ujao.
Ngoma ametua Azam akitokea Yanga aliyoichezea kwa takribani misimu miwili na waliachana naye mwanzoni mwa mwezi Mei kutokana na makubaliano maalumu likiwemo suala la majeruhi.