Ngassa awatumia salamu wanaowabeza Yanga

Muktasari:

Ngassa amesema kikosi cha Yanga kinaundwa na wachezaji wenye uwezo na kwamba hilo watathibisha uwanjani.

Morogoro.Winga mpya wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema kama kuna watu wanadhani timu hiyo imepoteza dira basi watanyamaza ligi ikianza.

Ngassa amesema kikosi cha Yanga kinaundwa na wachezaji wenye uwezo na kwamba hilo watathibisha uwanjani.

Amesema kwa sasa wamepewa mbinu nyingi tayari kwa mechi zao na kwamba watafanya makubwa kwa klabu yao tofauti na wanavyodhaniwa.

Aidha mkongwe huyo amesema ushindani wa namba katika kikosi chao ni mkubwa ambao utaipa mafanikio timu hiyo.