Neymar adhihirisha ubora wake Barcelona mbele ya Juventus

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya kirafiki ya maandalizi ya msimu iliisha kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao yote ya Barcelona yalifungwa na Neymar.

Marekani. Mshambuliaji Neymar ameifungia Barcelona bao la kwanza katika dakika ya 15 ya kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Juventus uliopigwa nchini Marekani.

Mechi hiyo ya kirafiki ya maandalizi ya msimu iliisha kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao yote ya Barcelona yalifungwa na Neymar.

Wiki hii kumekuwapo na taarifa za mchezaji huyo kuhamia PSG ambao wamemtangazia dau nono. Hata hivyo mchezaji huyo aliungana na timu yake kwenye mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey.