Ndolanga alia na Simba, Yanga kushindwa kuendeleza soka la vijana nchini

Muktasari:

  • Alisema ili soka la Tanzania liweze kuwa na heshima kwenye viwango vya Fifa, lazima waandaliwe vijana na wajengewe uzoefu tangu wakiwa wadogo.

Mwenyekiti wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga amezitaka klabu kongwe za Simba na Yanga kuonyesha ukomavu wao kwa kuanza kuandaa chipukizi katika timu zao vijana.

Alisema ili soka la Tanzania liweze kuwa na heshima kwenye viwango vya Fifa, lazima waandaliwe vijana na wajengewe uzoefu tangu wakiwa wadogo.

"Ifikie hatua viongozi wa timu hizo wabadilike, soka la kisasa linaelezwa kwa vijana. Hiyo ipo kwa nchi zote ambazo zimeendelea na siyo kusajili sajili kutoka nje ya nchi," alisema.

Ndolanga, alisema kuna vipaji vikubwa nchini, lakini mwisho wa siku vinakosa mwelekeo na kuishia kujulikana mitaani na siyo kitaifa kisha kimataifa.