Ndanda FC yachekelea ushindi wa ugenini

Monday September 11 2017

 

By Geofrey Kahango

Mbeya. Kocha Mkuu wa Ndanda, Mussa Mbaya amesema walijiandaa kisaiokojia kwamba walikuwa ugenini hivyo walihitaji kucheza kwa kujihami na kutafuta nafasi nzuri za kupata ushindi.

Timu hiyo jana imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mbeya City ushindi ambao unawapa mwelekeo katika mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema, “Tumepata ushindi ugenini sio kitu rahisi, lakini tunashukuru tumepata nafasi kadhaa na moja imetupa ushindi mapema kabisa na kazi kubwa ilikuwa kwanza kulinda lile bao na kutafuta nafasi nyingine ya kuongeza bao.”