Naibu Waziri Shonza amlilia Mzee Majuto

Dar es Salaam. Naibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema kifo cha Mzee Majuto ni pigo kubwa katika tasnia ya filamu nchini.
Akizungumza kwenye Ukumbi wa Karimjee, Waziri Shonza alisema kifo hiki ni funzo kwamba pamoja na jitihada ambazo binadamu yeyote anaifanya uhai ni kudra ya Mwenyezi Mungu.
“Wasanii pamoja na serikali ilijitolea katika kuokoa maisha ya Majuto wakati akiwa anaugua, lakini ndio hivyo jitihada haziwezi kuzidi kudra za Mwenyezi Mungu.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa watu wanaoingia mikataba na wasanii kufuata taratibu.
Waziri Shonza amewahakikishia familia yake kufuatilia haki zote za mzee Majuto kwa kazi ambazo aliingia mikataba na watu mbalimbali.