Mwimbaji wa Injili ashauri ishu ya Diamond, naibu waziri

Muktasari:

Sakata la Diamond na naibu waziri liliingiliwa kati na Balaza la Sanaa Tanzania (Basata) na kufafanua jambo hilo kwa undani.

 Katibu Mkuu  wa Tanzania Gospel, Foundation, Stella Joel amesema kwamba suala ambalo lilijitokeza hivi karibuni baina ya msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnamz kurumbana na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza ni vyema  suala hilo likamalizwa kwa kukaa meza ya mazungumzo.

Mwimbaji huyo wa Injili ambaye pia ni kiongozi umoja huo wa wasanii, alisema kwamba ni vyema kabla ya Serikali kuchukua hatua ikaangalia upya namna ya kukaa na wasanii na kuwapa elimu kuhusu kutunza maadili ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwaeleza kwa nini wanakataza wasiimbe wakiwa utupu.

Aidha, alisema changamoto kubwa ambayo bado wasanii wanakabiliwa nayo ni kutofaidika na kazi zao za sanaa kwani wajanja wachache wamekuwa wakiwanyonya.