Mwamichezo wa Tanzania apotea Australia

Monday April 16 2018

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Mcheza tenisi ya meza, Fathiya Pazi amezamia nchini Australia siku chache kabla ya kufungwa michezo ya Jumuiya ya Madola Jana Jumapili.

Fathiya ni miongoni mwa wanamichezo wa Tanzania waliokuwa wanashiriki michezo ya madola alitoweka kwenye kijiji cha michezo tangu Ijumaa iliyopita.

Mkuu wa msafara wa Tanzania, Yusuph Singo alikiri mchezaji huyo kutoweka na kubainisha kwamba tukio hilo wameriripoti polisi mjini Goldcoast.

"Ameondoka na begi lake dogo, begi kubwa na suti za michezo ameziacha, kama hadi kesho atakuwa ajarejea sisi tutaondoka na tutaichia polisi suala lake," alisema Singo.

Pazi anakuwa mwanamichezo 15 kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Rwanda na Cameroon walizamia Australia baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.