Mwakyembe amlilia Bisongo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe

Muktasari:

Bisongo alifariki dunia Aprili 18 katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanamuziki wa dansi Kalambay Bisongo.

Bisongo alifariki dunia Aprili 18 katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimesikitishwa na taarifa hizi za kifo cha mwanamuziki mahiri wa dansi, msiba huu ni pigo kwa Taifa na sanaa ya muziki,” alisema Dk Mwakyembe.

Enzi za uhai wake Kasongo alifanya kazi za muziki katika bendi za Tanzania one, Achigo na baadaye kuhamia bendi ya wazee sugu ya Kukumbi  Mwanza Mpango (King Kiki).

Dk Mwakyembe pia ametoa pole kwa familia, uongozi wa bendi ya wazee sugu wanamuziki wote wa dansi, chama cha muziki wa dansi Tanzania (Chamudata) ndugu jamaa na marafiki.