Mwadui kumaliza hasira kwa Mbeya City

Muktasari:

Mwadui hivi sasa ina pointi tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo minne na kushinda mmoja na kupoteza mitatu.

Dar es Salaam. Nahodha wa Mwadui, Awadh Juma amesema wanajisikia vibaya kupoteza mchezo dhidi ya Prisons nyumbani tena kwa mabao mengi.

Mwadui hivi sasa ina pointi tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo minne na kushinda mmoja na kupoteza mitatu.

Awadh alisema ni jambo baya kupoteza mechi ya tatu mfululizo lakini hawakati tamaa bali wanajipanga na kuangalia wapi wanakosea ili kuhakikisha wanarudi kivingine katika mchezo ujao.

"Haya matokeo yametuumiza sana kwa sababu tumefungwa mabao mengi halafu tuko nyumbani lakini inabidi tukubaliane na hali halisi na kusonga mbele.

Mwadui itashuka tena uwanjani Jumamosi kucheza na Mbeya City katika mchezo utakaofanyika kenye Uwanja wa Mwadui Compex Shinyanga.