Muungano wa Marekani, Canada Mexico kuandaa Kombe la Dunia 2026

Wednesday June 13 2018

 

Uswisi. Muungano wa Marekani, Canada na Mexico umeshinda tenda ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2026 na kuiangusha Morocco ambayo nayo iliomba nafasi hiyo.
Morocco imepata kura 65 sawa na asilimia 33 wakati Muungano wa Canada, Mexico na Marekani umepata kura 134 ambazo ni sawa na 67 asilimia.
Awali, Morocco iliahidi kuwa iwapo itapata uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2026, ingeipa FIFA kiasi cha Dola 5 billioni (Sh 10 trilioni) kama faida itakayopatikana kwenye mashindano hayo.
Muungano wa Marekani, Canada na Mexico umeshinda tenda ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2026 na kuiangusha Morocco ambayo nayo iliomba nafasi hiyo
Zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kumpata muandaaji wa Kombe la Dunia 2026, litaendeshwa kwa mfumo wa Kielektroniki.
Pia Ushirika wa Marekani, Canada na Mexico awali uliahidi kutoa faida ya Dola 11 bilioni (Sh 22 trilioni) kama faida ambayo FIFA itapata baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia iwapo utapata nafasi ya kuandaa fainali hizo mwaka 2026.