Mtendeni FC yaushika ubingwa Moro Kids

Muktasari:

Matokeo ya mechi hiyo ndiyo itakayotoa nafasi ya 515 KJ FC kutwaa ubingwa au la

Morogoro. Mbio za kusaka bingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Morogoro utaamuliwa kesho kwa mchezo kati ya Moro Kids FC na Maafande wa 515 KJ FC wilaya ya Kilosa mkoani hapa.

Maafande wa 515 KJ tayari imeweka matumaini ya kutwaa ubingwa huo baada ya jana (juzi) kuitandika Mtendeni FC bao 2-1 na kufikisha pointi tisa huku ikiomba dua mbaya kwa Moro Kids FC ipoteze mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mtendeni FC kesho ili kutwaa ubingwa huo.

Moro Kids yenye pointi saba itahiji kushinda mchezo huo ili kufikisha pointi 10 ili kutwaa ubingwa wa mkoa huo kwa mara ya kwanza na kuzima ndoto za wapinzani wao.

Mratibu wa taasisi ya kukuza na kuendeleza soka mkoani Morogoro (Moro Youth), Rajab Kindagule alisema kuwa wachezaji wao wamechukulia michezo ya ligi hiyo kama fainali na mchezo wa mwisho na Mtendeni FC utatoa mwanga kwa wachezaji wa taasisi hiyo kuendelea kujitangaza kwenye michezo ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

Kindagule alisema kuwa kiu ya taasisi ya Moro Youth ni kuona vijana wanacheza kwa kujituma dhidi ya Mtendeni FC na kupata ushindi ili kutwaa ubingwa wa mkoa wa Morogoro na kucheza ligi ya mabingwa wa mikoa na kusaka nafasi ya kutinga ligi daraja la pili Tanzania msimu ujao.

“Nina imani wachezaji, benchi la ufundi la Moro Kids litauchukulia mchezo huo na Mtendeni FC kama mchezo mkubwa kwani mchezo huo kwetu utatoa mwanga kwa taasisi huu ya Moro Youth na vijana kiujumla kuendeleza kuonyesha

Makamu Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA), Jimmy Lengwe alisema kuwa ligi hiyo itahitimishwa kesho kwa mchezo kati ya Moro Kids na Mtendeni FC saa 10 jioni kwenye uwanja wa Azimio.

“Bingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Morogoro msimu huu utaamuliwa na Moro Kids kesho (leo) baada ya kumalizika kwa mchezo wa mwisho dhidi ya Mtendeni FC yenye pointi tatu.”alisema Lengwe.