Mtanzania apambana timu isishuke daraja Ligi Kuu Kenya

Sunday November 12 2017

 

By ELIYA SOLOMON

BEKI wa Kitanzania anayeichezea Chemelil Sugar ya Kenya, Aman Kyata ameweka wazi kuwa kama wasingejituma kwenye michezo yao kadhaa ya hivi karibuni wangekuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Chemelil Sugar haipo kwenye hatari ya kushuka daraja tena hata kama itapoteza mchezo wao ujao wa kufunga pazia la Ligi Kuu Kenya kwa kucheza na Western Stima, Novemba 18.

"Yani pointi zetu na hao ambao wapo kwenye hatari ya kushuka ni chache, tuna pointi 39 kwenye nafasi ya 11, waliopo kwenye nafasi ya 12 hadi 14 nao wana pointi kama zetu,nafasi zile tatu za mwisho timu zilizopo zina pointi kuanzia  25 hadi 35.